Hesabu 12:1-15 ONEN - Bible AI

1Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi.

2Waliuliza, “Je, Bwana* amesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” Naye Bwana* akasikia hili.

3(Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)

4Ghafula Bwana* akawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njooni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda.

5Kisha Bwana* akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele,

6Bwana* akasema, “Sikilizeni maneno yangu:

7Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;

8Kwake nitanena naye uso kwa uso,

9Hasira ya Bwana* ikawaka dhidi yao, akawaacha.

10Wakati hilo wingu liliinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia, akaona ana ukoma.

11Kisha Aroni akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu.

12Usimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”

13Hivyo Mose akamlilia Bwana* akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”

14Bwana* akamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.”

15Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.

>