Yeremia 45:1-4 ONEN - Bible AI

1Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruku mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruku kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule:

2“Hili ndilo Bwana*, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruku:

3Ulisema, ‘Ole wangu! Bwana* ameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”

4Bwana* akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana*: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kungʼoa kile nilichokipanda katika nchi yote.

>