1Ee Bwana*, nimekukimbilia wewe,
2Nitegee sikio lako,
3Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,
4Uniepushe na mtego niliotegewa,
5Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako,
6Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili;
7Nitafurahia na kushangilia upendo wako,
8Hukunikabidhi kwa adui yangu
9Ee Bwana* unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida;
10Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi,
11Kwa sababu ya adui zangu wote,
12Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa,
13Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi;
14Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana*;
15Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,
16Mwangazie mtumishi wako uso wako,
17Usiniache niaibike, Ee Bwana*,
18Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe,
19Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,
20Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako
21Atukuzwe Bwana*,
22Katika hofu yangu nilisema,
23Mpendeni Bwana* ninyi watakatifu wake wote!